HATIMAYE FILAMU YA MAXIMO YANBGA SC YAFIKIA TAMATI


HATIMAYE filamu ya ujio wa aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mbrazil Marcio Maximo kujiunga na klabu ya Yanga imefikia tamati jana baada ya uongozi kutarajia kumtangaza kocha mpya wiki ijayo. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga Mwesiga Selestine alisema kocha huyo atatoka katika nchi zilizopo Amerika Kusini au Ulaya. 
Alisema uongozi ulipitia maombi ya makocha 25 waliotuma wasifu zao kwa ajili ya kutaka kibarua katika klabu hiyo ambapo wamewachuja na kubaki watano. 
Akizungumzia suala la Maximo, Katibu huyo alisema wameamua kuachana naye kwa vile bado ana mkataba na klabu yake ya Democrata FC ya Rio de Janeiro,Brazil huku pia akipata ofa za kufundisha timu mbalimbali za Taifa ikiwemo timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’. 
“Kwa sababu hizo isingekuwa rahisi kumchukua Maximo kufundisha Yanga, kwa mantiki hiyo tumeshafanyia mchujo maombi na kubaki makocha watano ambapo mmojawapo ndiye atakayekuja kuinoa Yanga,”alisema. 
Hivi karibuni Yanga ilitangaza ujio wa Maximo nchini kwa ajili ya kurithi mikoba ya Mserbia Kostadin Papic ‘Clinton’ ambaye alitupiwa virago miezi michache kabla ya kumaliza mkataba wake kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio timu hiyo. 
Hata hivyo kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ujio wa Maximo  ulibaki kuwa ‘kiza kinene’ huku uongozi ukishindwa tena kuweka wazi kilichosababisha kocha huyo ashindwe kutua nchini kama walivyotangaza awali. 
Katika hatua nyingine,kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Kaunda chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro, ikiwa ni maandalizi ya michuano ya kagame inatotarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 14.

Comments

  1. WANAYANGA TUPOOOOOOO?MAXIMO KAOTA MBAWA OOOOH AWEZI KUJA ANAMKATABA,SI TULIAMBIWA ANAKUJA J'PILI
    NA TICKET KATUMIWA,VP SASA KUHUSU TICKET YETU,...?INA MAANA WAKTK WANASEMA ANAKUJA JPIL WALIKUWA HAWAJUWI KAMA ANAMKATABA?VP JAMANI WANAYANGA BADO HAMJASTUKIA KAMA KUNA PICHA LINACHEZWA HAPA....ANYWAY KAMA WANAWEZA KUTU SAUNDISHA MAXIMO ANAKUJA KUMBE ANAMKATA JE HATUONI KAMA HAWA MAJAMAA WANATUONA SISI MABWEGE?SASA KAMA LEO WAMETUTANGAZIA JAMAA ANAMKATABA MBONA JUZI AKILI MAVI ALISEMA SHAFII DAUDA NDIO KAMZUHIA ASIJE,?SASA TUAMINI NINI NA NANI KT YA HAO,?JAMANI VIONGOZI WA YANGA WAACHE KUCHONGA CHONGA OVYO WASITUCHUKULIE POA.

    ReplyDelete
  2. Mbona wana yanga wenyewe wanaelewa? kwani ni ajabu mtu kumchumbia mwanamke na akamkosa? Yanga walimtaka Maximo lakini kutokana na mikataba yake imeshindikana, cha ajabu ni nini? acheni kushikia bango ishu za wenzenu, angalieni simba yenu.

    ReplyDelete

Post a Comment