VPL:YANGA YASHINDA DAR, SIMBA YABANWA TANGA

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga Sc hii leo wameondoka na pointi tatu baada ya kuitandika Rhino ya tabora mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aidha mahasimu wao wa jadi Simba Sc ambao leo walikuwa ugenini mjini Tanga wakikwaana na wenyeji Coastal Union wamejikutwa wakibanwa mbavu na kulazimishwa sare tasa.
Yanga ambayo ushindi wa leo umepoza machungu ya sare ya mabao 3-3 waliyoipata dhidi ya mahasimu wao Simba jumapili iliyopita, iliutawala mchezo huo ambapo ilipata ushindi wake kupitia kwa  Hamis Kiiza aliyefunga mawili na Frank Domayo aliyefunga bao moja.
Mbali na mechi hizo, hii leo kulikuwa na mtanange mwingine uliozikutanisha Tanzania Prisons ya Mbeya dhidi ya Kagera Sugar ambapo Kagera imeshinda bao 1-0.