SWAHILI FASHION WEEK KUFANYIKA DESEMBA 5 HADI 8@GOLDEN TULIP


 Meneja Maboresho Swahili Fashion Week, Hamis K Omary akizungumzia uboreshwaji wa Swahili Fashion Week 2013
 
Maonesho ya sita ya Swahili Fashion Week yatafanyika Golden Tulip Hotel kuanzia tarehe 5 mpaka 8 Desemba 2013, Dar Es Salaam, Tanzania. 
Swahili Fashion week 2013 itakusanya wabunifu 40 kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuonesha mitindo yao, yenye kwenda na wakati na kutegemewa kushika soko la Afrika Mashariki mwaka 2014.
“Swahili Fashion Week mwaka huu ina lengo la kuifikia jamii zaidi, na kukuza vipaji katika tasnia ya mitindo. Ni zaidi kuhusu kuthamini wabunifu wa kwetu na kuwatengezea jina,huku tukiwapeleka ngazi za juu zaidi kila mwaka” Akizungumza Bw. Washington Benbella, Meneja wa Swahili Fashion Week. 
Ukiwa ni mwaka wa 6 wa Swahili Fashion Week, Katika mashindano ya wabunifu wanaochipukia, Waandaaji wamependekeza dhima ya mwaka huu (theme) “Evolution” ambayo inawataka wabunifu chipukizi hao kubuni mavazi yanayoashiria mabadiliko, si lazima upya, ila yenye muonekano wa kitofauti na mzuri. 
“Tunasisitiza jamii iunge mkono tasnia ya mitindo na kuvaa mavazi ya kikwetu, hasa kwa Tanzania. Vipaji vya nyumbani vinahitaji kukuzwa ili kufikia majina yanayotambulika duniani katika tasnia hii. Hisani huanza nyumbani, na ndio maana tunategemea kampuni pamoja na mashirika mbali mbali kusaidia tasnia ya mitindo” Hamis K Omary, Meneja Masoko Swahili Fashion Week.
Swahili Fashion week imedhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel, Eventlites, Push Mobile, BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa), Ultimate Security, Global Outdoor Ltd na 361 Degrees.

Comments