KUELEKEA UCHAGUZI WA TFF:JAMAL MALINZI KUZINDUA KAMPENI ZAKE J'5@SERENA HOTEL


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Awali ya yote nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wajumbe wa kamati ya uchaguzi ya TFF kwa juhudi zao na umakini katika kusimamia mchakato uchaguzi mkuu wa TFF 2013.
Aidha naomba nichukue fursa hii kuwafahamisha wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na wadau wa mpira wa miguu nchini kuwa nitazindua rasmi ilani yangu ya uchaguzi siku ya jumatano Tarehe 23/Octoba/2013 kuanzia saa tano asubuhi katika hoteli ya SERENA iliyopo mtaa wa ohio. Mialiko kwa wanahabari ya kuhudhuria uzinduzi huu italetwa punde kwenye vyombo vya habari.

Nichukue fulsa hii kuwatakia kila  la kheri wagombea wote, niwatakie kampeni njema, kampeni zenye wingi wa baraka na fanaka tele, na nina imani tutafanya kampeni za kistarabu zisizo onyesha hisia za ubaguzi wa aina yoyote iwe wa dini, kabila, jinsia au ueneo, lengo letu kuu liwe ni kujenga hoja za msingi tukijielekeza ni kwa vipi tutakabiliana na changamoto zinazoukabili mpira wetu.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki TFF.
 Jamal Malinzi

Mgombea nafasi ya Uraisi uchaguzi w TFF 2013