SIMBA SC YAWATOA NISHAI MABINGWA WA SOKA ZANZIBAR

WEKUNDU wa Msimbazi Simba Sc jioni ya leo wamewatoa nishai mabingwa wa soka Visiwani Zanzibar, KMKM baada ya kuitandika mabao 2-1, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao timu zote ziliutumia kwa ajili ya kujiandaa na michezo yake ya ligi ambapo Simba inashiriki ligi kuu bara na huku KMKM ikishiriki ligi ya Visiwani Zanzibar.
Simba ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Said Ndemla, kabla ya Mrundi Gilbert Kaze kuandika la pili ambapo timu hizo zilikwenda mapumziko kwa Simba kuongoza mabao 2-0.
Ikiwa na wachezaji wake mahiri wakiwemo Ali Shiboli na Abdi Kassim,KMKM inayonolewa na Ally Bushir ilionekana kujipanga zaidi katika kipindi cha pili hivyo kujipatia bao pekee kupitia kwa iddi Kambi.