SIMBA SC YAITANDIKA MAFUNZO 4-3

WEKUNDU wa Msimbazi,  Simba Sc leo wameitandika Mafunzo ya Zanzibar mabao 4-3 katika mchezo wa kujipima nguvu uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo, pamoja na Simba kushinda mchezo huo lakini haikuonesha kandanda safi kama ilivyotarajiwa na mashabiki wake huku Mafunzo ikionesha kandanda safi na ya kuvutia.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba Mrundi Amisi Tambwe aliiandikia Simba mabao mawili, huku mengine yakifungwa na Sino Augustino pamoja na Nassoro Masoud 'Cholo'
Wakati Simba iliutumia mchezo wa leo kutambulisha wachezaji wake wapya watatu kwa mashabiki wa jiji la Dae es Salaam, sambamba na kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Septemba 14, Mafunzo iliutumia mchezo huo kujiweka sawa kwa ajili ya Ligi Kuu ya Zanzibar iliyoanza leo Visiwani humo.