MTIBWA SUGAR:HATUJAKATA TAMAA LIGI NDIO INAANZA

LICHA ya kutopata matokeo mazuri  katika michezo yake ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara, klabu ya ya Mtibwa Sugar ya Manungu, Morogoro, imesema haijakata tamaa kwani ligi hiyo ndio kwanza mbichi.
Mtibwa Sugar ambayo jioni hii inashuka katika dimba la Sokoine Mbeya kukwaana na wenyerji Tanzania Prisons, tangu kuanza kwa ligi hiyo ambayo leo inaingia katika raundi ya tano imeshinda mechi moja tu dhidi ya ndugu zao Kagera Sugar ilipowafunga bao 1-0.
Aidha, Mtibwa ilitoka sare tasa na Mbeya City, kabla ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na Azam Fc na kisha kutandikwa mabao 2-0 na Simba sc.
Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime amesema kwamba matomkeo waliyoyapa ni sehemu ya mcheszo hivyo hayawezi kumkatisha tamaa na hasa ikizingatiwa kwamba ligi ndiyo mwanza imeanza.
Alisema kikosi chake kipo vizuri na kitaendelea kujipanga zaidi kwa ajili ya michezo ijayo ya ligi hiyo.
"Utashangaa wanaoshinda sasa baadaye ndio watakuja kuwa chini zaidi ya sisi tunaoshindwa sasa, matokeio ya sasa hayatuvunji moyo kwani safari ndiyo inaanza,"alisema Mecky naodha wa zamani wa Taifa Stars.