CHEKA ATINGA DODOMA, KUPONGEZWA BUNGENI KESHO

BINGWA wa dunia wa ndondi WBF Francis Cheka amewasili mjini Dodoma leo ambapo kesho atatambulishwa rasmi bungeni sambamba na kupongezwa.
Cheka aliyetwaa ubingwa huo ijumaa iliyopita baada ya kumtwanga Mmarekani Phil Williams, amekwenda Dodoma kwa mwaliko wa Waziri wa habari utamaduni, Vijana na Michezo Dk.Fenella Mukangara.