YANGA YAANZA NA HAMSA VPL, SIMBA, AZAM FC ZABANWA UGENINI

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga Sc leo wameanza vizuri kutetea ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuwatandika wauza mitumba wa Ilala, Ashanti Fc kwa mabao 5-1.Mchezo huo ulifanyima katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Aidha,mahasimu wao wa jadi Simba Sc waliokuwa wageni wa Rhino Fc mjini Tabora, walijikuta wakibanwa mbavu na kutoka sare ya mabao 2-2, mchezo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini humo.
Makamu Bingwa wa Ligi hiyo, Azam Fc nao wamekikuta wakishindwa kufurukuta mbele ya wakata miwa wa Manungu, Mtibwa Sugar baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kupitia mchezo uliorindima Uwanja wa Manungu, Turiani.
Mchezo mwingine wa ufunguzi wa ligi hiyo ulikuwa baina ya Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar na kupigwa katika uwanja wa Sokine mjini Mbeya ambapo timu hizo zilitotoka sare tasa.
Nao Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga wameweza kuwatambia maafandande wa JKT Oljoro baada ya kuwatandika mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Maafande wa JKT Ruvu nao wametoka kifua mbele mbelke ya maafande wenzao Mgambo Shooting ya Tanga baada ya kuwatandika mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa dimba la Mkwakwani jijini Tanga, huku maafande wa Ruvu Shooting nao wakiibuka wababe dhidi ya wenzao Tanzania Prisons ya Mbeya kwa kuifunga mabao 3-0 mchezo uliofanyika uwanja wa mabatini, Mlandizi.