UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BODI YA LIGI TANZANIA (TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD) – TPL BOARD KUFANYIKA OKTOBA 18

1. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa Tanzania Premier League Board utafanyika tarehe  18 Oktoba 2013 jijini Dar es salaam. Wajumbe wa Baraza la TPL Board wanaopenda kuwania nafasi za uongozi wa TPL Board wanataarifiwa  kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TPL Board zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi tarehe 20 Agosti 2013 katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF ( Idara ya  Fedha), kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha Fomu ni saa 10:00 Alasiri tarehe 20 Agosti, 2013.

2.  Nafasi zinazotangazwa kugombewa ni hizi zifuatazo:

(i)                   Mwenyekiti  wa  TPL Board.
(ii)                 Makamu Mwenyekiti wa TPL Board.
(iii)                Wajumbe wawakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board (TPL Board Management Committee), nafasi mbili (2).

3.                   Mtu yeyote  anayeomba nafasi ya uongozi katika TPL Board lazima atimize masharti yafuatayo:

(i)                   Awe Raia wa Tanzania
(ii)                 Awe na kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu elimu ya Sekondari.
(iii)                Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)               Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)                 Awe na umri wa angalau miaka 21.
(vi)               Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(vii)              Kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa TPL Board awe Mwenyekiti wa kati ya Klabu zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya sita kwenye Ligi Kuu kwa msimu uliopita (2012/13).
(viii)            Kwa nafasi za  Mjumbe mwakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board awe Mwenyekiti wa Klabu Daraja la Kwanza.

4.                   Ada za Fomu za maombi ya uongozi ni hizi zifuatazo:

(i)                   Mwenyekiti  na Makamu Mwenyekiti wa  TPL Board; Shillingi Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).
(ii)                 Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPL Board; Shillingi Laki moja (Tshs. 100,000/=).

5.Kwa wale ambao walilipia fomu za kugombea katika mchakato uliofutwa na ambao wanakusudia kugombea nafasi zile zile walizozilipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.

6. Ratiba ya mchakato wa Uchaguzi wa TPL Board imeainishwa hapa chini:

Na.
TAREHE
SHUGHULI

1.

14/08/2013
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutangaza Uchaguzi wa TPL Board, nafasi za kugombea na sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.

2.

16/08 /2013 – 20/08/2013
Kuchukua Fomu za maombi ya uongozi wa TPL Board kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Katibu Mkuu wa TFF). Fomu zitatolewa kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 10.00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha fomu kwa Katibu Mkuu wa TFF ni Jumanne tarehe 20/08/2013 saa 10:00 Alasiri.

3.

21-23 /08/2013
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia fomu za waombaji uongozi wa TPL Board. Kutangaza matokeo ya upitiaji fomu na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo majina ya waombaji uongozi wa TPL Board (23/08/2013).

4.

24/08/2013-26/8/2013
Kutoa fursa ya pingamizi kwa waombaji uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 26/08/2013 saa 10:00 Alasiri. Pingamizi ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF. Pingamizi zizingatie matakwa ya Ibara ya 11(3) ya Kanuni za Uchaguzi.

5.

27/8/2013- 29/08/2013
Wawekaji Pingamizi na waliowekewa Pingamizi kuitwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa utetezi wao kuhusu Pingamizi. Kamati kujadili Pingamizi.

6.

30/08/2013 - 03/09/2013
. Usaili na kutangaza matokeo ya pingamizi na ya usaili / Kuwajulisha kwa maandishi wagombea matokeo ya usaili. Kutangaza orodha ya awali ya wagombea
7.
04 – 06/09/2013
Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF kuwasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili, kwa kujadiliwa na kutolewa maamuzi na Kamati ya Maadili ya TFF.

8.

04 – 06/09/2013
Kutoa fursa ya kukata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF (TFF Elections Appeal Committee) kwa masuala yasiyo ya Maadili. Rufaa zilizoambatanishwa na ada ya malipo ya Rufaa zitapokelewa na Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 06/09/2013 saa 10:00 Alasiri.

9.

07-13/09/2013
Kamati ya Maadili ya TFF kupitia mashauri yote yanayohusu  Maadili na kuyatolea uamuzi.

10.

14- 16/09/2013
Kamati ya Maadili ya TFF kutoa matokeo ya maamuzi ya mashauri ya maadili kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF na wagombea.

11.
17- 19/09/2013
Kukata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 19/09/2013 saa 10:00 Alasiri


12.

20- 24/09/2013
Kusikiliza Rufaa zilizopelekwa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF na kutolea uamuzi.

13.

25-27 /09/2013
Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kuwafahamisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Wagombea matokeo ya Rufaa zilizosikilizwa na Kamati ya Rufaa ya Maadili
   14.
28/9/2013 – 2/10/2012
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi kusikiliza rufaa za uchaguzi wa TPL Board kwa masuala yasiyo ya Maadili.
   15.
03-04/10/2013
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kutangaza na kuwapa taarifa za matokeo ya rufaa wagombea waliokata rufaa (zisizohusu mashauri ya Maadili).  Aidha Kamati ya Uchaguzi ya TFF nayo kufahamishwa matokeo ya rufaa hizo.
     16.
05/10/2013
Kutoa orodha ya wagombea wote waliopitishwa kugombea uongozi wa TPL Board na kuwataarifu  wajumbe wa Baraza la TPL Board.
     17.
06/10/2013-17/10/2013
Kipindi cha  kampeni kwa wagombea wote
      18.
18/10/2013
Uchaguzi wa viongozi wa TPL Board


7.                Uchaguzi wa TPL Board unafanyika kwa mujibu wa Kanuni za uendeshaji za TPL Board na Kanuni za Uchaguzi za TFF.


Hamidu Mbwezeleni
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF