MSIBA WAAHIRISHA SHOO YA SIKINDE ILIYOKUWA IFANYIKE JIONI YA LEO LITTLE THEATRE

Uongozi wa Kivuli Entertainment inapenda kuwataarifu wapenzi wa muziki wa dansi kwamba show ya Mlimani Park Orchestra 'Sikinde' ambayo ilipangwa kufanyika leo Ijumaa kuanzia saa 1 jioni imelazimika kuhairishwa kutokana na msiba wa mfanyakazi mmoja mwandamizi wa The Little Theatre, pahali ambapo show hiyo ilitakiwa kufanyika.
Kutokana na taarifa hizo, Kivuli Entertainment inaungana na menejimenti ya The Little Theatre kwa kuondokewa ghafla na mfanyakazi mwenzao Bi. Grace. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Mwisho, tunapenda kuomba radhi kwa wapenzi wote wa muziki wa dansi kwa usumbufu uliotokea. Kivuli Entertainment itatoa tarehe mbadala wa lini show hii itafanyika. Ahsanteni.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano - Kivuli Entertainment