YANGA, YATOKA SARE NA MABINGWA WA UGANDA

MABINGWA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga leo wametoka sare ya bao 1-1  na mabingwa wa Uganda,  Kampala City Councel (KCC) katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kirafiki, Yanga ilianza kutikisa nyavu za KCC kupitia kwa kiungo wake mpya, Hamis Sadick kabla ya Kavu Mawini  kusawazisha dakika chache baadaye.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ameshukuru viwango vilivyooneshwa na wachezaji wake na  hasa ikizingatiwa kuwa walicheza na mabingwa wenzao.
Brandts alisema ameona viwango walivyonavyo wachezaji wake hivyo atafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.

Timu hizo zitarudiana kesho mjini Shinyanga katiika mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa kambarage mjini humo, kabka ya kuelekea mjini Bukoba kucheza na timu watakayopangiwa na wenyeji wao.