YANGA SC YATUA JIJINI MWANZA LEO


Kikosi cha Mabingwa wapya wa Ligi Kuu nchini Tanzania bara timu ya Young Africans leo mchana wametua kutua katika jiji la mwanza tayari kabisa kwa ziara yake ya wiki moja kanda ya ziwa ambapo kesho inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya mabingwa wa Ligi nchini Uganda KCC dimba la CCM Kirumba.
Yanga inaondoka mchana wa leo kuelekea jiji la Mwanza kwa shirika la ndege la Ndege la Precion Air ambapo jioni inatarajia kufanya mazoezi mepesi katika uwanja wa CCM Kirumba tayari kabisa kujiandaa na mpambano huo wa hapo kesho.
Kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema anafurahi kupata nafasi hiyo ya kutembelea kanda ya ziwa, wapenzi na washabiki watapata fursa ya kuwaona wachezaji wao na kusherekea ubingwa.
Katika ziara ya kanda ya ziwa Yanga itakua na mcihezo mitatu ya kirafiki ambapo mchezo wa kwanza utafanyika CCM Kirumba jijini Mwanza, jumapili uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na mchezo wa mwisho utafanyika alhamis uwanja wa Ally Hassana Mwinyi mjini Tabora.
Yanga inaondoka na msafara wa watu 34 ikiwa  na kikosi cha wachezaji 23 na benchi la ufundi na viongozi watatu. 
CHANZO:www.youngafricans.co.tz