UMOJA WA WATANZANIA NCHINI UJERUMANI KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADUNI



 Watayarishaji wa Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg,nchini Ujeruamani,wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayoanza 19 hadi 21 Julai 2013.
Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana sana na shughuli za Umoja wa Watanzania ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania,wandaaji wa onyesho hilo wametoa nafasi kwa umoja wa Watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.

Mwenyekiti wa UTU Bw.Mfundo Peter Mfundo (pichani)ameupokea mwaliko huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi Ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na watanzania, Umoja wa Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.
Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na

Comments