SHAMRASHAMRA ZA UFUNGAJI WA KOMBE LA DIWANI BONNA KATIKA PICHA

 Charles Baba, Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa akitumbuiza baada ya mashindani ya Diwani Bonnah Cup yaliyomalizika mwishoni mwa wiki. Anaye pga makofi ni muuandaji wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonnah Kaluwa katika viwanja vya Social Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.
 Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonnah Kaluwa akifurahi kwa kucheza baada ya mashindano aliyoandaa ya Bonnah Cup yaliyoshirikisha zaidi ya timu 20, Anayeimba ni Charles Baba Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa katika viwanja vya social  Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.
 Charles Baba Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa akiimba wimbo wa risasi kidole uliokonga nyoyo za wapenzi wa muziki baada ya mashindano ya Diwani Bonnah Cup katika viwanja vya social Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.
 Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakicheza katika viwanja vya Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki baada ya baada ya kumalizaika kwa mashindano ya Diwani Bonnah Cup ambapo timu ya stakishari ilikuwa mabingwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi ikimpa mfano wa zawadi ya hundi ya shs laki tatu Kapteni wa timu ya Vipaji halisi Hassani Juma ambapo timu yao ilikuwa mshindi wa pili wa mashindano hayo ya Bonna Cup kwenye picha katikati ni Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonna Kaluwa.
 Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonna Kaluwa akifurahi kwa kucheza mziki ulikuwa ukipolomoshwa na bendi ya Mashujaa katika viwanja vya Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi ikimpa mfano wa zawadi ya hundi ya shs laki moja mfungaji bora wa mashindano hayo.