OWINO, WALULYA KUIBEBA URA KESHO IKIIVAA SIMBA U/TAIFA

 NYOTA wa Uganda waliopata kukipiga katika klabu ya Simba, George Owino na Derick Walulya kesho wanatarajiwa kuingoza timu ya URA ya Uganda katika mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Simba.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki unatarajiwa kupigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam ambapo tayari timu hizo zimewasili jijini Dar es Salaam tayari kabisa kwa pambano la kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati Simba ikiwasili jana kutoka mikoani ilipokwenda kwa ziara maalum ya kimichezo katika mikoa ya Tabora, KAtavi, Shinyanga na Mara, URA yenyewe imetokea kwao Uganda 


Pambano hilo ambalo litatoa fursa kwa mashabiki wa Simba kuwashuhudia nyota wapya waliosajiliwa kutoka ndani na nje ya nchi, litaanza majira ya saa kumi kamili jioni.

MSIBA
 KWA niaba ya Kamati ya Utendaji ya Simba, Wanachama na Wapenzi wa klabu, Mhe; Rag anatoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mzee Juma Urongo aliyefariki dunia asubuhi ya leo na kutarajiwa kuzikwa leo jioni huko Tandika jijini Dar es Salaam.
Mzee Urongo alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wazee la Simba na ni miongoni mwa kizazi cha wazee walioanza kuishabikia klabu tangu ikiitwa Sunderland.
Rage amesema binafsi atakosa sana busara, ushauri na maelekezo yam zee huyo ambaye alikuwa shabiki wa Simba katika nyakati nzuri na mbaya.

Mungu na aiweke mahali pema roho ya marehemu Juma Urongo.