NSAJIGWA APATA ULAJI LIPULI FC YA IRINGA

HATIMAYE kozi ya awali ya ukocha aliyoipata nahodha wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’ imezaa matunda baada ya kupata kazi ya kuifundisha klabu ya Lipuli ya mjini Iringa inayoshiriki Ligi daraja la kwanza.
Nsajigwa aklikuwa ni mmoja ya wahitimu wa kozi hiyo iliyoandaliwa na chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kumalizika wiki iliyopita.
Mwenyekiti wa Lipuli Abuu Changawa amesema kwamba  wamemchukua Fusso kutokana na uzoefu wa kucheza muda mrefu katika klabu ya Yanga pia ni mmoja ya wachezaji wenye nidhamu hivyo atasaidia kuwaweka wachezaji katika nidhamu nzuri.

Alisema wamedhamiria kuhakikisha timu yao inautoa kimasomasoa mkjoa wa Iringa ambao kwa zaidi ya miaka 10 umeshindwa kutoa timu katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.