KUNDI LA NDEGE WATATU NDIYO HABARI YA MUJINI


 Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa. 
Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3
KUNDI jipya la muziki  lijulikanalo kama Ndege 3 limeanzishwa rasmi huku  likiundwa na wanadada  wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo.
Tayari kundi hilo  hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho tayari kimeanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

 Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.