JOSEPH OWINO AMWAGA WINO SIMBA SC


HATIMAYE beki wa kati  Mganda Joseph Owino amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea klabu ya soka ya Simba.
Habari kutoka Simba zinaeleza kwamba Owino ambaye alikuwa akichezea URA ya Uganda amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba.
Ikumbukwe kuwa, Owino alipata kuichezea Simba miaka ya nyuma kabla ya kumuacha baada ya kuandamwa na majeruhi ya muda mrefu na kisha klabu ya Azam Fc kumsajili.
Aidha, baada ya kuondoka Azam FC Owino alitua URA.