DIAMOND, KALA JEREMIAH, SNURA KUPAGAWISHA MOSHI KESHO KATIKA TAMASHA LA KILI

 Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya nembo yake  ya  Kilimanjaro  Premium  Lager,  inaendelea na ‘Kili Music Tour 2013’ wikiendi hii mjini Moshi.
Tamasha hili  kubwa  litafanyika Jumamosi ya tarehe 06 Julai, 2013,  mjini Moshi kwenye kiwanja cha Ushirika na litajumuisha wasaniii 10 ambao ni Barnaba,Diamond, AT, Snura Mushi, Professor J, Lady Jay Dee, Roma, Kala Jeremiah, Joh Makini na Ben Pol.
“Tunashukuru kuwa watanzania wamepokea tamasha hili kwa vizuri kabisa na wameshiriki kikamilifu kwenye mikoa ya Dodoma na Tanga, hivyo basi tunategemea Moshi itajumuika nasi ipasavyo kufanikisha tamasha litakalofanyika mkoani hapo Jumamosi ya tarehe 06.” Alisema bwana George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro.
Bwana Kavishe aliendelea kufafanua kuwa “bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kutoa bonge la kiburudisho kwa watanzania kwa kuhakikisha kuwa kila mkoa unapelekewa wasanii mahiri kabisa wa muziki wa bongo fleva wawaburudishe “kikwetukwetu”
Msanii wa muziki nchini Tanzania Diamond alinukuliwa akisema kuwa “ kama kawaida yangu nimejiandaa ipasavyo kuhakikisha kuwa ninawaburudisha mashabiki wangu ipasavyo. Hivyo basi msikose kuhudhuria na kujionea ufanisi mahiri wa Diamond Platnumz.”
Matamasha ya Kili Music Tour 2013 yatapumzika kwa muda wa mwezi mmoja na kurejea tena kuanzia tarehe 17 Agosti, 2013 kwenye mikoa mitano iliyobaki.