BI. KIDUDE AENZIWA TAMASHA LA ZIFF

Na Andrew Chale, Zanzibar
 
WANAMUZIKI Nguli nchini wakiongozwa na  Sit bin Saad ambaye ni mjukuu wa marehemu Bi.Kidude,Synerg,Baby J wote hawa ni kutoka Zanzibar  Linah na THT Band kutoka Dar es Salaam kesho watawasha moto ndani ya mabo klabu kwa ajili ya  kumuenzi marehemu Bi.Kidude ambaye aliwahi kutumbuiza katika matamasha ya ZIFF yaliyowahi kufanyika. 
Tamasha la filamu la nchi za Jahazi maarufu kama ZIFF linaendelea kupamba moto na kesho ni usiku maalumu wa wanawake katika kumuenzi  marehemu Bi.Kidude katika tamasha hilo. 
Tamasha hilo ambalo lina siku ya 5 tangu kuanza kwake limekuwa ni kivutio kikubwa kwa wakazi na wageni kutoka kila kona ya dunia  kuwapa burudani kulingana na mahitaji.
 
Usiku  wa wanawake unatarajia kufanyika jioni ya leo ndani ya Mambo klabu ampapo wasanii watakao tumbuiza katika tamasha hio watakuwa ni wanawake pekee  ambapo  mjukuu wa marehemu Bi.KIdude atafungua dimba kutoa  burudani hiyo.
 
Wanawake wameombwa kuhudhuria kwa wingi kwakuwa  tamasha la siku ya leo ni kwa ajili ya wanawake.
 
 katika tamasha hilo la usiku wa wanawake wasanii hao wataweza kukonga nyoyo za mashabiki wake na kufanya kufana kwa tamasha hilo ambalo linamkumbuka Bi.kidude kwa mchango wake ambao alikuwa akiutoa katika kipindi chake chote cha uhai wake.
 
Hata hivyo burudani hiyo itaambatana na kuonyeshwa kwa filamu mbili tofauti ikiwemo ya The Last Fishing Boat kutoka Malawi na Lilet never Happened kutoka Netherland.