TWANGA PEPETA, BEN POL KUPAMBA SHINDANO LA MISS TEMEKE 2013

BENDI ya muziki wa dansi wa Twanga Pepeta na mwanamuziki wa kizazi kipya Ben watapamba shindano la Miss Temeke 2013.
Shindano hilo limepangwa kufanyika Julai 5, katika ukumbi wa TCC Club Chang’ombe ambapo jumla ya warembo 16 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.
Mkurugenzi wa BMP Promotions, ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Ben Kisaka, alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea vizuri.
Kisaka alisema warembo wanaowania taji hilo wanaendelea na mazoezi makali kabla ya kupanda jukwaani wakiwa chini ya wakufunzi Suzan Mwenda na Shadya Mohamed.
Shindano la Redds Miss Temeke, litakuwa linafanyika siku chache tu kabla ya mfungo wa Ramadhan, hivyo ni kama vunja jungu kwa wale wataoingia katika mfungo. Warembo 16 wamekuwa wakiendelea na mazoezi chini ya wakufunzi Suzan Mwenda na Shadya Mohamed.
Warembo hao ni pamoja na Aksaritha  Vedastus ,Irene Rajab, Darline Mmary, Esther Muswa   Hyness  Oscar, Latifa Mohamed, Jamila Thomas, Margreth Rajab, Magdalena Olotu, Mey Karume,Mutesa George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface, Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, City Sports Lounge, Blogu ya Wananchi, RIO Quality Gym &Spa, Fredito Entertainment na Kitwe General Traders. Temeke, imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali.
Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi yapili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.

Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.

Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.

Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions

Comments