SIMBA YAACHANA NA SAMUEL SENKOOM

SIMBA imeamua kuachana na beki Mganda Samuel Ssenkoom (pichani )baada ya kutoridhishwa na kiwango chake tangu ajiunge na timu hiyo Juni 4 mwaka huu kwa ajili ya majaribio. 
Habari za uhakika kutoka Simba ambazo Sports Lady Blog imezipata zinaeleza kwamba,tayari uongozi umeshamkatia tiketi ya bus la  tayari kumrejesha kwao nchini Uganda.
Kiongozi mmoja wa Simba amesema kwamba Senkoom anatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kuanzia sasa baada ya kushindwa kuonesha kiwango cha kuridhisha tangu atue nchini kwa majaribio. 

Ssenkoon aliyeanza  kujinoa na wenzake Juni 5 kupitia mazoezi yanayoendelea kwenye uwanja wa Kinesi, ameshindwa kuonesha makali kama ilivyotarajiwa huku kocha mkuu wa Simba Abdallah ‘King’ Kibaden kwa nyakati tofauti alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa haridhishwi na kiwango cha Mganda huyo ambaye alikuwa nakipiga katika klabu ya URA.