KOCHA BRANDTS AMKATAA YAW BERKO, DIDA ACHUKUA NAFASI

HATIMAYE ndoto za kipa wa Kimataifa Mghana Yaw Berko kuendelea kuichezea klabu ya Yanga zimefikia tamati baada ya kusajkiliwa kwa kipa mzawa, Deogratius Munishi 'Dida'.
Hiyo imetoa jibu la utata uliuokuwa umetanda ndani ya klabu hiyo baada ya Berko kumaliza mkataba wake mwezi Mei na hivyo viongozi kuwa katika mjadala juu ya kumuongeza ama kutomuongeza mkataba mpya.
Hata hivyo, habari ambazo Sports Lady Blog imezipata kutoka Yangfa zinaeleza kuwa, kocha mkuu wa klabu hiyo Ernie Brandts ndiye aliyekataa kuobngezwa mktaba kwa Berko na badala yake kubariki usajili wa Dida.
Berko ambaye alijiunga na Yanga mwaka juzi hakuweza kuichezea klabu hiyo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu bara msimu uliomalizika baada ya kwenda nchini Congo kujaribu kujiunga na klabu ya FC Liupopo ya huko ambayo ilipanga kumbadili na beki, Kabange Twite.
Hata hivyo mazungumzo juu ya kubadilishana huko wachezaji hayakufikia muafaka na ndipo Lupopo ilipomchukua Twite na Berko kurejea nchini kuendelea kusubiri hatima yake.
Kusajili kwa dida kunafanya Yanga kufikisha makipa watatu baada ya Ali Mustafa ;'Barthez' na  Yusuf Abdallah ambaye amepandishwa toka kikosi cha Vijana cha Yanga