KILI MUSIC TOUR NI ZAMU YA TANGA JUMAMAMOSI HII

Dar es Salaam, Tanzania, Juni 27, 2013:  Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya nembo yake  ya  Kilimanjaro  Premium  Lager,  inaendelea na  tamasha  lingine kubwa  la muziki lijulikanalo kama ‘Kili Music Tour 2013’ wikiendi hii mjini Tanga.
Tamasha hili  kubwa  litafanyika Jumamosi ya tarehe 29 Juni,  2013 mjini Tanga kwenye kiwanja cya Mkwakwani na itajumuisha wasaniii 8 ambao ni Ally Kiba, Snura Mushi, Professor J, Mwana FA, Recho, Mzee Yusuph, Roma na Kala Jeremiah.
Tamasha hili lililokuwa linajulikana kama KTMA Winners Tour mwaka huu lilibadilishwa jina na kuwa Kili Music Tour ili kupanua uwigo wake na  kujumuisha wasanii walioshinda tuzo za Kili Tanzania Music Awards, wasanii waliopendekezwa kwenye tuzo na wasanii ambao hawakushiriki kwenye tuzo lakini ni vinara kwenye tasnia ya muziki nchini.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bwana George Kavishe alinukuliwa akisema “tumeona ni jinsi gani mkoa wa Dodoma uliitikia wito na kushiriki kwa kikamilifu kwenye Kili Music Tour wikiendi iliyopita, hivyo basi tunategemea Tanga itajumuika nasi ipasavyo kufanikisha tamasha litakalofanyika mkoani hapo Jumamosi ya tarehe 29.”
Bwana Kavishe aliendelea kufafanua kuwa “mwaka huu ndani ya staili ya “kikwetu kwetu” bia ya Kilimanjaro Premium Lager inahakikisha kuwa kama kawaida inatoa bonge la kiburudisho kwa watanzania ikizingatia jinsi watanzania tunavyojivunia mambo yetu ya kitofauti kama muziki wetu wa bongo fleva, dansi yetu ya kiduku, kandanda letu lenye ushabiki wa simba na yanga, lugha yetu ya kipekee na bia yetu ya Kilimanjaro iliyotengenezwa Tanzania, kwa kutumia viungo vya kitanzania na watanzania.”
Msanii aliyebobea wa bongo flava ajulikanaye kama Professor J (Joseph Haule) naye alisema “wakazi wa Tanga na vitongoji vyake wasubiri shoo kubwa ya kufana kama waliyoipata wakazi wa Dodoma wiki iliyopita. Tunategemea kuwashangaza wanatanga kwa kuwapa vionjo ambayo hawajawahi kuviona kwani mimi na wasanii wenzangu tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa hatuwaangushi mashabiki wetu na kuwa tutawapa bonge la kiburudisho!”          

                            

Comments