KABANGE TWITE ATIBUA ULAJI WA YAW BERKO, VIONGOZI YANGA WAGAWANYIKA

UONGOZI wa klabu ya Yanga umegawanyika kuhusiana na kumuongeza mkataba aliyekuwa kipa wake wa kimtaifa Mghana Yaw Berko.
 Berko aliyejiunga na Yanga mwaka 2009 akitokea klabu ya Liberty Proffessional ya Ghana , mwaka jana ilikuwa ajiunge na klabu ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) lakini ikashindikana. 
Hiyo inatokana na uongozi wa klabu hizo mbili kutofikia muafaka kwani ilikuwa Berko aende kule na beki Kabange Twite aje kuichezea Yanga lakini ilishindikana na kila klabu kuamua kumchukua mchezaji wake. 
Hata hivyo, baada ya zoezi hilo kushindikana Berko ameendelea kuwa nje ya kikosi cha Yanga licha ya kuwepo hapa nchini akisubiri hatima yake ndani ya klabu hiyo.
 Sports Lady Blog ilipomtafutaKatibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako kutaka kuhusaina ana suala la kipa huyo, alisema lipo mikononi mwa kamati ya usajili ambayo baada ya kukamilika kwake itatoa taarifa rasmi. 
“Suala hili lipo kwa kamati ya usajili nadhani wao ndio wenye mamlaka zaidi ya kujua kama ataongezwa mkataba ama la na baada ya hapo ndipo watatupa taarifa uongozi,”alisema 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb alikiri suala hilo kuwapo mezani kwao na kwamba muda si mrefu litapatiwa ufumbuzi. 
Alisema kilichotokea ni kutotimia kwa maelewano baina ya Fc Lupopo na Yanga juu ya Berko na hivyo ilibidi nyota huyo arudi nchini kwani alikuwa bado na mkataba ndani ya Yanga. 
Berko aliyekuwa kipa namba moja wa Yanga, baada ya kuondoka kwake nafasi yake ilichukuliwa na Ally Mustafa ‘Barthez’ ambaye alionesha umahiri mkubvwa kiasi cha kuiwqezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2012/2013. 
Kwa sasa Yanga ina makipa wawili tu, Barthez na Yusuf Abdalla ambaye amepandishwa kutoka timu ya Vijana ya Yanga.


 

Comments