HIKI NDICHO KILICHOMFUKUZISHA KASEJA SIMBA SC

  Na Dina Ismail
PAMOJA na kutowekwa wazi sababu rasmi ya kuachwa kwa kipa Juma Kaseja, imebainika kwamba ni kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao Yanga.
Simba ilipokea kipigo hicho, katika mchezo wa funga dimba wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Mei 18 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Kaseja Ndiye aliyekaa langoni.
Sports Lady Blog imezinyaka habari za kuaminika toka ndani ya uongozi wa Simba zinaeleza kwamba, kitendo kile kimewaudhi sana viongozi kwani mabao aliyofungwa yalionbekana dhahiri kuwa yalitokana na uzembe wake.
Kiongozi mmoja wa Simba aliliambia gazeti hili kwamba, pamoja na mapungufu yote aliyonayo Kaseja lakini walikerwa  zaidi na kufungwa kwake.
“Hivi unavyomfahamu wewe Kaseja anaseweza kufungwa mabao kama yale, kwa kweli hilo limetacha na maswali mengi kichwani, imetkera sana mwache aende zake,”alisema
Akienda mbali zaidi, kiongozi huyo ingekuwa vizuri zaidi kama Kaseja angeweza kuonesha umahiri wake na kuondoa dhana mbovu dhidi yake, lakini kitendo cha kukubali nyavu zake kutikiswa kilitoa jawabu juu ya maswali walitokuwa nayo.
Hivi karibuni kumekuwa na utata juu ya Kaseja kusajiliwa tena kwenye kikosi cha Simba baada ya mkataba wake kumalizika huku baadhi wakitaka aongezwe na wengine wakipinga.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage, Kaimu Makamu Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na Mwenyekiti wa kamati ya usajili, zakaria Hanspoppe kwa nyakati tofauti walisema Kaseja hawezi kuongezwa mkataba.
Viongozi hao walitoa kauli hizo bila ya kueleza wazi sababu za kumuacha kipa huyo namba moja wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambaye ameitumikia klabu hiyo karibu miaka 10.

Huku hayo yakiendelea, Kaseja mwenyewe ameendeklea kukaa kimya na hata alipotafutwa kuzungumzia hilo hakuwa tayari.