DORICE MOLLEL ATWAA TAJI LA MISS TABATA 2013


Miss Tabata Dorice akipozi na Mshindi wa pili Upendo Lema (kulia) na Mshindi wa tatu Recho Mushi (kushoto).
Na Mwandishi Wetu
Mwamafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Kumbumbumbu ya Mwalimu Nyerere Dorice Mollel (22) usiku wa kuamkia jana alishinda taji la Miss Tabata kwenye shindano lililofanyika katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata.
Dorice aliwabwaga  warembo wengine 14 kumrithi Noela Michael aliyekuwa anashikilia taji hilo. Noela ndiye anayeshikilia taji la Miss Ilala kwa sasa.
Mshindi huyo alizawadiwa Sh 600,000 na king’amuzi kutoka Multichoice pamoja na warembo waliyoshika tano za juu watawakilisha Tabata katika shindano la Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Warembo hao ni Upendo Lema (22) aliyezawadiwa sh 400,000 baada ya kushika nafasi ya pili na Recho Mushi (20) alipata Sh 300,000 baada ya kushika nafasi ya tatu. Wengine ni Kazunde Kitereja (19) alishinda nafasi ya nne na kuzawadiwa Sh 200,000 na Kabula Juma Kibogoti (20) alipataSh 150, 000 kwa kushika nafasi ya tano.
Warembo wengine waliyoingia kumi bora kila moja alipata shilingi laki moja. Nao ni Madgalena Bhoke (21), Eunice Nkoha (19), Rehema Kihinja (20), Brath Chambia (23) na Joaniter Kabunga (21). Warembo waliyosalia walipata kifuta The rest got consolation prize of Sh 50,000 each.
Miss Tabata iliandaliwa na Bob Entertainments na Keen Arts chini ya udhamini wa Dodoma Wine, Redd’s Original, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.