BAADA YA KUIPOTEZEA MICHUANO YA KAGAME, YANGA KUANZA KUJINOA JUMANNE IJAYO


Wachezaji wa Yanga wakisherehekea Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013

Baada ya kuwa na mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji wake na benchi la Ufundi, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2012/2013 timu ya Young Africans Sports Club itaanza mazoezi wiki ijayo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa 2013/2014.
Wachezaji wote na benchi la ufundi wataanza mazoezi siku ya jumanne julai 02 saa 2 asubuhi katika uwanja wa shule ya Sekondari Loyola kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom ambayo inatarajiwa kuanza agosti 24, 2013.
Kocha Mkuu Ernie Brandts ambaye yupo kwao nchini Uholanzi kwa mapumziko ya wiki mbili, anatarajiwa kurejea siku ya jumatatu julai mosi usiku kisha siku ya jumanne ataongoza mazoezi hayo kwa kushirikiana na kocha msaidizi Fred Felix Minziro.
Yanga inaanza mazoezi mapema ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuhakikisha inatetea ubingwa wake na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, awali Yanga ilianza mazoezi june 3 kujianda na mashindano ya kombe la Kagame ambalo serikali ilizizuia timu za Tanzania kushiriki mashindano hayo kutokana na hofu ya usalama nchini Sudan..






CHANZO:www.youngafricans.co.tz

Comments