NYOTA LIGI KUU BARA WAALIKWA MAFIA

BAADHI  ya wachezaji nyota  wa ligi kuu soka Tanzania Bara mwishoni mwa wiki hii watakwenda Wilayani Mafia kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo katika wilaya hiyo.
Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa mabingwa wa soka wa Wilaya hiyo El itihad ambapo wakiwa huko watacheza mechi kadhaa za kirafiki.
Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Haruna moshi 'Boban', Juma Nyoso, Amir Maftah, Shaban Kado, Nurdi Bakari, Shaaban Kisiga, victor Costa, Mussa Mgosi, Chacha Marwa, Rasmadhan Chombo 'redondo', Jerry Tegete, Deogratias Munish 'Dida'Shadrack Nsajigwa na wengineo.