MSANII WA BONGO FLEVA JOSLIN AREJEA UPYA KWENYE FANI

JOSLIN

BAADA ya kimya cha muda mrefu msani wa bongo fleva aliyepata kutikisa miaka ya nyuma kupitia kundi la Wakali kwanza, Joslin ameibuka upya kwenye medani hiyo ambapo ametoka na singo inayokwenda kwa jina la 'ITIKA'
Joslin ambaye single ya 'NIITE BASI' ilipata kumuweka  matawai ya juu kwenye medani ya muziki huo ameiambia Sports Lady kwamba singo yake hiyo ameitayarisha kwenye studio za One Love Fx chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter.
"Nawaomba mashabiki wangu mnipokee kwa mikono miwili kupitia singo yangu hii ambayo naamini imejitosheleza katika kila Idara,"alisema.