KHADIJA KOPA, BANANA ZORO KUMTOA MISS UKONGA JUMAMOSI HII


MALKIA wa mipasho nchini pamoja na B Band inayoongozwa na msanii Banana Zorro wanatarajiwa kutoa burudani katika shindano la kumsaka  Redd's Miss Ukonga, linalotarajiwa kufanyika Mei 25 mwaka huu katika Ukumbi wa Wenge Garden, Ukonga.
Mratibu wa shindano hilo, Rashid Kazumba alisema jana kwamba maandalizi kwa ajili ya shindano hilo litakaloshirikisha warembo 17 yanaendelea vema, huku washiriki wakiendelea kujifua.
“Maandalizi yote yameshakamilika kwa kiasi kikubwa ambapo tunatarajia kuwa mashindano yatakuwa ya aina yake kwani warembo wana sifa na tumedhamiria kumtoa Miss Tanzania kutoka katika Kitongoji chetu” alisema
 Kazumba aliwataja baadhi ya warembo watakaopanda jukwaani kuwa ni pamoja na Happyness Jackson, Flosek Mwakanyamale, Glory Jigge, Annatolia Raphael, Musnat Hassan, Gift Swai, Natasha Mohamed, Vanessa Magule, Queen John, Martha Gewe, Nancy Obasi, Mwanamkasi Bakari  na Diana Joachim.
Aidha, Kazumba aliwaomba mashabiki wa urembo wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya shindano hilo ambapo kiingilio kitakuwa sh. 8000 kwa viti vya  kawaida wakati  VIP watalipa sh.15,000.
Shindano hilo limedhamniniwa na kinywaji cha  Redd's ambao ni washamini wakuu, Z. Entertainment, Uefa Go City Pub, Mamushka Catering, Break Point, Saluti 5, Times FM, Clouds FM, Business Times, Hiltec Resort pamoja na Kiota Jungle.