Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) inakutana Mei 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam kupokea na kupanga
utekelezaji wa maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
kuhusu uchaguzi wa shirikisho.
Kikao hicho cha dharura chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF,
Leodegar Tenga kitakuwa na ajenda hiyo moja tu katika kuhakikisha utekelezaji
wa maelekezo ya FIFA unafanyika haraka ili uchaguzi ufanyike ndani ya muda
uliopangwa.
FIFA katika maelekezo yake imetaka kwanza ziundwe Kamati ya
Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili kabla ya kuingia kwenye mchakato wa
uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF. FIFA imeagiza uchaguzi uwe
umefanyika kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.
Comments
Post a Comment