Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) inakutana Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kupitia maandalizi ya Ligi
ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyopangwa kuanza Mei 12 mwaka huu.
Tayari mikoa 18 kati ya 27 kimpira imeshapata mabingwa wao
kwa ajili ya RCL itakayotoa timu tatu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014).
Kamati hiyo chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia
ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF itapokea taarifa ya maandalizi ya ligi
hiyo kutoka Idara ya Mashindano ya TFF na kufanya uamuzi juu ya mikoa ambayo
haijawasilisha mabingwa wao.
Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na
ratiba (draw) itapangwa wakati wowote. Ada ya kushiriki ligi hiyo kwa kila
klabu ni sh. 100,000 na usajili utakaotumika na ule ule wa ligi ngazi ya mkoa.
Hakutakuwa na usajili mpya wa wachezaji.
Comments
Post a Comment