WANAWAKE BONGO WAAMUA KUMTENGA DIAMOND

Na Jacob Buberwa
Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi.Wema Sepetu,
na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke" . kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kielekeza jamii kuishi
kwa kufuata na kuheshimu mahadili ,lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni kiongozi wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha
kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu ya kimapaenzi kati yake na
Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi.Penny,kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania" Tunaowaomba akinamama
na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video,vcd,cd
pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanya na mwamuziki
Nasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote
wa kitanzania popote pale walipo.
Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na
na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji wa Mwanamke"