VIDEO YA MUZIKI GANI YA NEY NA DIAMOND YAANZA KUREKODIWA

Ney na Diamond wakirekodiwa

MSANII wa muziki wa bongo Fleva anayekwenda Elibariki Munishi maarufu kama ‘Ney Wa Mitego’ ameanza kazi ya kurekodi video ya wimbo wake, Muziki Gani aliomshirikisha Nassib Abdul ‘Diamond’
 Ney ameiambia Sports Lady leo kwamba video ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake itarekodiwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. 
Alisema kazi ya kutayarisha video hiyo imefanywa na kampuni ya Visual Lab chini ya Adam Juma, hivyo amewataka mashabiki kukaa tayari kuipokea kazi hiyo pindi itakapokamilika.