Na
Mwandishi Wetu
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss
Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park,
Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga
amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha na mashindano
ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri
zaidi.
“Warembo wazuri wamejitokeza zaidi kuliko
mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje
na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen
Arts.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano
wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.
Warembo hao ni Pendo Judica Moshi (20),
Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19),
Upendo Dickson Lema (22), Martha Gewe (19),
Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally
(18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),
Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge
(18) na Sophia Claud (21).
Wengine ni
Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali
(21), Rafhel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy
Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim
Abass (22) na Shan Abass (22).
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa
kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda
ya Ilala.
"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote
anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu
liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki
mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa
Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Waliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni
Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
Comments
Post a Comment