Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa
mchezaji Yusuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji.
Shirikisho la Mpira wa Miguu cha Msumbiji (FMF) lilituma
maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela
Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo.
Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu (free agent)
amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya wachezaji
kumi kutoka Tanzania hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini
Msumbiji.
Comments
Post a Comment