NYOTA YANGA KUFANYIWA UPASUAJI, NURDIN AENDELEA VIZUR

BEKI wa kati wa klabu ya Yanga Ladisalus Mbogo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki ijayo katika hospitali ya Mwananyamala.
Kwa mujibu wa daktari wa klabu hiyo, Dk.Nassoro Matuzya beki hiyo atafanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe kwenye shavu lake.
Aidha, Dk. huyo aliongeza kuwa hali ya kiungo wa timu hiyo Nurdin Bakari aliyepata maumivu ya goti asubuhi ya leo kwenye mazoezi inaendelea vizuri.
Alisema baada ya Nurdin kufanyiwa uchunguzi ilibainika ni tatizo dogo tu linalohitaji dawa na hivyo kesho ataendelea na mazoezi na wenzake