Timu ya
Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa
Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi
ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Msafara wa
timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na
utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.
Siku hiyo
Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya
mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.
Wachezaji
walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri,
Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair,
Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na
Abdeljalil Jbira.
Issam El
Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada,
Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani,
Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na
Youssef El Arabi.
Wakati huo
huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa katika vituo vya
Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko
mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa
na Dar Live Mbagala.
Milango siku
ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana.
Comments
Post a Comment