MANYARA YASHINDA TAJI LA TAIFA MISS UTALII 2012/13 - VIPAJI

 Mshindi wa Tuzo la Vipaji akiwa anafuraha Muda Mchache baada ya kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi.
 Mshindi wa Miss Utalii  Vipaji kutoka Mkoa wa Manyara wa kati kati akiwa na washindi wenzake wawili waliofika mpaka Tatu bora



 Muheshimiwa Meya wa Manispaa ya Temeke Maabadi Suleiman Hoja Akimvisha tuzo la vipaji Mshindi kutoka Mkoa wa Manyara.

 Washiriki walio ingia tatu Bora wakiwa katika picha ya Pamoja na Mustaiki meya.


Hatimaye Mshiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kupitia mkoa wa Manyara wake imeshinda tuzo la vipaji 2012/13 na kuibwaga mikoa mengine wa mikoa 29 ya tanzania bara na zanzibar Mary 19 alionesha vipaji vya hali ya juu katika ushindani ambao
ulikuwa mkubwa hasa kutoka kwa warembo wa mikoa ya Lindi , Kagera, Dodoma, Zanzibar, Katavi, hata hivyo
mchuano ulikuwa mkali zaidi kati ya Miss Utalii, Lindi Manyara na Kagera ambao walionesha Umahili mkubwa wa kucheza ngoma za asili na kupelekea kuingia katika hatua ya Tatu Bora. Katika Hatua hiyo ya Tatu Bora washirika hao walicheza wimbo mmoja ujulikanao kwa jina la katope kutoka kundi la ngoma za asili la kibiriti ambao ni mchanganyiko wa ngoma mbalimbali wa makabila ya ngoma za kusini.
Katika Hali iliyo wafanya wapenzi wa Fani ya Urembo waliofulika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala kuto kuamini kwamba wanao cheza jukwaani ni Mabinti wa Kizazi kipya ambao kwa Hali ya kawaida  ya sasa ni nadra sana kumuona sister Duu tena Mrembo kucheza ngoma za asili kwa ufasaha na umahili mkubwa. hivyo kuwafanya wapenzi hao kuacha viti vyao na kuanza kushangilia kwa nguvu mwanzo hadi mwisho huku wakiwapongeza waandaaji wa shindano la Miss Utalii Tanzania kuwa ni Hazina kubwa ya utamaduni wa Mtanzania na Wengine  wakithubutu kusema Miss Utalii ni mtambo wa kurekebisha tabia kwa kuweza kuwabadirisha  fikra za mabinti hao wa kizazi kupya mashindano hayo kwa ya kuwa kucheza ngoma za asili ni ushamba hadi kuwafanya kuwa wacheza ngoma mahili tena hadhalani bila ya Aibu na kwa kujivunia utamaduni na Ngoma za Asili Tanzania. Wengi wa wapenzi waliohudhulia katika
shindano hilo wakisika kwa nyakati tofauti kuitaka na kuishauli serikali na mamlaka za utalii  kudhamini shindano la Miss Utalii Tanzania kwa Faida ya Jamii na Taifa  kwani shindano hili  limedhihilisha uwezo mkubwa wa sio  tuuu kuhifadhi utamaduni wa mtanzania bali pia kuhamasisha na kutangaza utalii wa tanzania kitaifa na kimataifa.  
Alisikika Mpenzi Mmoja aliye julikana kwa jina La Jafary Shaibu akisema kuwa shindano hili ni zuri na ni lakipekee lakini tatizo inaonekana waandaaji hawajapata wadhamini wa uhakika, kwanini Serikali isiwasaidie hawa? 
Akizungumza katika Shindano hilo ambalo Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao alikonga nyoyo za watu kwa Muziki wake wenye asili ya kitanzania, Mgeni Rasmi Muheshimiwa Maabad Suleiman Hoja Mustahiki Meya wa Manispaa ya Temeke aliwapongeza sana washiriki na washindi lakini alitoa shukurani za pekee kwa waandaaji wa mashindano haya kwa kuipa manispaa na wilaya ya Temeke Heshima kubwa ya kuwa wenyeji wa Tukio hili la kitaifa lenye hadhi ya jimataifa
alisema kwamba hii ni heshima kubwa kwa Manispaa ya Temeke wilaya ya Temeke Tunao uwezo na Hadhi kuwa wenyeji  wa matukio makubwa ya kimataifa na kitaifa kama hili la miss utalii tanzania 2012/13. Hivyo kutoa fulsa ya pekee kwa Temeke kujitangaza kitlii, kitamadunina kiuwekezaji  ndani na nje ya Nchi, aliahidi kuwa manispaa ya Yemeke inatawaunga mkono kwa Hali na Mali ili kufanikisha fainali hizo ambazo zitafikia kilele katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Dar es salaam pia aliwataka wadau mbalimbai kujitokeza kudhamini shindano hilo. 
Mshindi wa Tuzo hiyo ya Vipaji ambaye alishangiliwa na washiriki wote baada ya kutangazwa kama mshindi, alizawadia Scholarship ya kusoma kozi ya Kiwango  cha Diploma katika chuo chochote nchini.
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA ) www.misstourismorganisation. blogspot.com


Comments