MALKIA WA NYUKI KUONGOZA KAMATI YA USHINDI SIMBA SC



WAKATI baadhi ya uongozi wa Simba ukianza kumeguka, kamati ya utendajhi ya klabu hiyo imeunda kamati ndogo  ya ushindi ambayo itakuwa chini ya mwenyekiti wake, Rahma Al Kharoos ‘Malkia wa nyuki’(pichani)
Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba kamati ya utendaji ya klabu hiyo iliyokutana juzi, iliamu kuunda kamati hiyo kwa  kuzingatia kwamba bado ligi inaendelea na Simba ina mechi ngumu mbele ya safari,kwa lengo la kusaidia timu kufanya vizuri katika mechi zake zilizosalia.
Alisema mbali na Malkia wa wajumbe waliopo ndani ya kamati hiyo ni pamoja Sued Nkwabi, Joseph Itang’are Kinesi, Dan Manembe na Francis Waya.
Alisema  Kamati ya Utendaji ya Simba imeshtushwa na kujiuzulu kwa  Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange na Zacharia Hans Poppe, ambapo tayari za kujiuzulu kwao zimefika kwa Mwenyekiti na akiona maamuzi hayo yanafaa, ataamua kwa mujibu wa maslahi ya klabu.
“Kamati ya Utendaji imeshtushwa na kujiuzulu kwa wajumbe hao muhimu. Mchango wao ulikuwa bado unahitajika sana ndani ya klabu. Michango yao ya hali na mali ndani ya klabu katika miaka mitatu iliyopita ilikuwa chachu kubwa ya mafanikio yaliyopatikana,”alisema Kamwaga.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wapenzi na wanachana wa Simba kuwa watulivu katika kipindi hiki. Kamati yenu ya utendaji iko imara na inataka kuwahakikishia washabiki kwamba hali si mbaya kama inavyoonekana,”aliongeza Kamwaga.
Kamwaga aliongeza kwamba katika kipindi hiki ambapo Makamu amejiuzulu na Mwenyekiti yupo nje ya nchi kwa matibabu, kamati imeniteua Mzee Kinesi kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti hadi Mwenyekiti atakaporudi.
Katika ha tua nyingine, Kamati ya imeazimia kuanza mchakato wa mazungumzo na kundi la Mpira Pesa ambapo lengo ni kuhakikisha tunaondoa misuguano ya ndani kwa ndani baina yao kuweza  kuunganisha nguvu na kuokoa timu 

Comments