KILA LA HERI AZAM FC


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewatakia kila la heri wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF) katika mchezo wake wa keshokutwa dhidi ya wenyeji Barrack Y.C.II ya Liberia, 
Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura amesema leo kwamba wamepata taarifa toka kwa ofisa wa TFF aliyeambata na Azam Fc Liberia kwamba kikosi cha Azam kipo katika hali nzuri na wachezaji wamepania kushinda mchezo huo.

Alisema TFF inaamini Azama imefanya maandalizi ya kutosha hapa nyumbani kwa ajili ya mchezo huo ambao wanahitaji kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ili watakaporudiana nyumbani iwe rahisi kwao kushinda na hatimaye kusonga mbele.

Azam Fc inakutana na Waliberia hao baada ya kuwasukumiza nje kwenye michuano hiyo Al Nasr Juba ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 8-0.