KIIZA, DHAIRA NA UMONYI WAITWA UGANDA CRANES
KAMPALA, Uganda

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, Uganda Cranes, Bobby Williamson, ametangaza kikosi cha nyota 22 kitakachoikabili Liberia hapo Machi 24, wakiwemo nyota watatu wanaocheza timu za Yanga, Simba na Azam.
Kwa mujibu wa kikosi hicho ambacho kitaingia kambini Machi 17 kwa mechi hiyo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, nyota hao ni Hamis Kiiza wa Yanga, kipa Abel Dhaira wa Simba na Brian Umonyi wa Azam.
Aidha, Williamson amemwita kiungo wa zamani wa klabu ya Bunnamwaya, Boban Zirintusa anayekipiga katika klabu ya  Power Dynamos ya Zimbwabwe na Kizito Luwagga wa klabu ya Leixieos FC ya Ureno.
Wengine ni Denis Onyange wa klabu ya Mamelodi Sundown na kipa Abel Dhaira
wa Simba ya Tanzania na mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Daniel Sserunkuma aliyeifungia Uganda katika mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda, Februari mwaka huu.
Uganda itakwaana na Liberia wiki mbili zijazo mjini Monrovia ikikamia ushindi kujiweka nafasi nzuri kwenye kundi lake la J, ikiwa nafasi ya pili kwa pointi mbili nyuma ya Senegal yenye pointi 4 huku Angola ikiwa ya tatu kwa pointi 2 na Liberia pointi moja.
Katika kikosi hicho, kocha Bobby amemwita Patrick Ochan, aliyekosa mkwaju wa penalti katika mechi ya mwisho ya kuamua timu ya kucheza fainali za Kombe la Afrika dhidi ya Zambia na Martin Mutumba anayecheza soka nchini Sweden.
Timu hiyo itaanza mazoezi yake Machi 17 katika uwanja wa Taifa wa Mandela, mjini
Namboole.

Kikosi kamili 
Makipa: Denis Onyango (Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini), Dhaira (Simba, Tanzania)  na Hamza Muwonge (Vipers SC)
Mabeki: Denis Guma (SCVU), Simeon Masaba (URA FC), Joseph Ochaya (Asante Koto, Ghana), Henry Kalungi (Railhawks, USA) Isaac Isinde (St. George Ethiopia), Nicholas Wadada (Vipers), Godfrey Walusimbi (CS Don Bosco, DRC), Andrew Mwesigwa (FC Ordabasy, Kazakhstan).
Viungo: Boban Zirintusa (Power Dynamos, Zimbabwe), Kizito Luwagga (Leixieos, Portugal), Said Kyeyune (URA FC), Mike Mutyaba (TP Mazembe, DRC) and Tony Mawejje (free agent), Musa Mudde (Simba SC), Hassan Wasswa (KCC FC), Geoffrey ‘Baba’ Kizito (Sai Gon, Vietnam), Moses Oloya (Vietnam)
Washambuliaji: Kiiza (Yanga, Tanzania), Daniel Sserunkuma (Gor Mahia, Kenya), Geoffrey Massa (Yenicam, Cyprus), Brian Umony (Azam, Tanzania), Emmanuel Okwi (Etoile Du Sahel, Tunisia)