JESHI LA YANGA SC LATINGA MJI KASORO BAHARI, LAWASUBIRI KWA HAMU MAAFANDE KESHO


Kikosi cha Young Africans Sports Club
Timu ya Young Aficans ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya Polisi Morogoro katika muendelezo wa michezo ya VPL mzunguko wa pili, mchezo utakaofanyika majira ya saa 10  jioni katika dimba la uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Baada ya kuichapa timu ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 katika mchezo wake wa mwisho uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa, Yanga jana jioni imewasili mjini Morogoro tayari kabisa kwa ajili ya kuwakabili vijana wa afande Mwema katika mchezo utakao kuwa na ushindani mkubwa.
Young Africans ambayo tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Vodacom, imecheza michezo saba (7) huku ikishinda michezo sita (6) na kutoka sare mchezo mmoja, hivyo kuweza kujikusanyia jumla ya ponti (alama) 19 kati ya zote 21.
Mpaka sasa Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa na pointi 48 na mabao 37 ya kufunga na mabao 12 ya kufungwa, ikiwa ni pointi 8 mbele ya timu ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 40.
Mara baada ya kuwasili mjini Morogoro, kocha mkuu wa Yanga mholanzi Brandts amesema anashukuru kikosi chake kimefika salama, wachezaji wote wapo katika hali nzuri ya mchezo hivyo anaamin timu yake itafanya vizuri katika mchezo wa kesho.
"Nafahamu timu ya Polisi ipo katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi, inahitaji pointi ili kuwez kujinusuru iishuke daraja, najua watacheza kwa nguvu kuhakikisha wapate pointi, lakini sisi pia tutacheza kwa nguvu na umakini mkubwa kuhakiisha hatupotezi mchezo huo" alisema Brandts
Yanga imewasili mjini Morogoro ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 ambao ni:
Ally Mustafa 'Barthez' na Yusuph Abdul (magolikipa)
Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Juma Abdul, Godfrey Taita, Nadir Haroub 'Cannavaro' (walinzi)
Nurdin Bakari, Frank Domayo, Athuman Idd 'Chuji, Nizar Khalfani, David Luhende (viungo) 
Said Bahanuzi, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete na Saimon Msuva (washambuliaji)
mchezaji Haruna Niyonzima ameshindwa kuungana na timu katika safari ya Morogoro kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia, Omega Seme na golikipa Said Mohamed wakiwa majeruhi, huku Geroge Banda na Rehani Kibingu wakibakia kuendelea na mazoezi na timu ya U-20.
CHANZO.www.youngafricans.co.tz