HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MACHI 21 HADI 23@PATHENON HALL


Meneja Biashara wa Harusi Trade Fair Hamis Omary Akizungumza na wandishi wa habari , kulia kwake ni Mustafa Hassanali.

Maandalizi  ya Harusi Trade Fair 2013 yapamba moto, Maonyesho hayo ya wafanyabiasharas wa bidhaa na huduma za harusi yanatarajiwa kuanza tarehe 21 machi hadi tarehe 23 machi katika viwanja vya ukumbi wa pathenon uliopo mkabala na Red Cross barabara ya Ali Hassan Mwinyi Upanga Dar es salaam. Muanzilishi na muandaaji wa Harusi Trade fair Mustafa Hassanali amesema ikiwa ni mwaka wake wanne maonesho haya yamekuwa na kuongezeka ubora ukilinganisha na miaka iliyopita halikadhalika tunatarajia kuona mabadiliko kwenye tasnia ya Harusi na washikadau wake.
Mwaka huu Harusi Trade Fair tayari imeshawavuta washiriki wengi wengi wao ni washirikia ambao wapo toka kuanziswha kwa maonyesho haya mwaka 2010.
Maonesho hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu yatakuwa yakianza saa 4;00 asubuhi na kumalizika saa 1:00 jioni.
“Harusi ni muunganiko wa familia na jamii na nikumbukumbu muhimu ya itakayodumu maisha yote, hivyo basi tumeamua kuwapa bibi na bwana harusi watarajiwa mahitaji yao yote ya siku hiyo muhimu kwenye hitoria ya maisha yao.” Amesema ndugu Hamis Omary meneja  miradi wa 361 degrees ambao ndio waandaaji wa onesho hilo.
Harusi Trade Fair inawaleta pamoja wadau wa biashara za harusi ili waweze kukutana kufahamiana na kuangalia fursa za kibiashara baina yao ili waweze kuzitumia kuboresha biashara zao na uhusiano wa kibiashara  ambao utachangia kukuwa kwa tasnia hii.
Miongoni mwa washiriki amabao watakuwepo mwaka huu ni pamoja na keki, maua na wapambaji, wapiga picha, wabunifu wa mavazi ya harusi na wengineo wengi.
“Kwakuwa idadi kubwa ya washiriki imethibitisha ushiriki wao, tunawaomba na kuwashauri watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kuona na kuthamini ubunifu wa bidhaa za Kitanzania “ alimalizia ndugu Omary.
Maonyesho hayo ya biashara za Harusi yameletwa kwenu kwa hisani ya 361 degrees, Clouds Fm and Clouds Tv, Global Outdoor system, Ultimate security, Prime advitising, Century  Cinemax na Vodacom
-- 
Mustafa Hassanali
Managing Director