FID Q, DA STAMINA KUSHEREHESHA COCO BEA CH SIKU YA PASAKA


Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanatarajiwa kushuhudia burudani ya kipekee kutoka kwa wasanii  wa muziki wa kizazi kipya Fid Q na  Da Stamina  katika tamasha Mahususi lililoandaliwa kwa ajili ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam siku ya jumapili ya pasaka.
Tamasha hilo litakalo fanyika katika Fukwe za bahari ya Hindi maarufu kama (coco Beach) linatarajiwa kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es Salaam kwa kutuo burudani hiyo bure kupitia tamasha lililoandaliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.
Akizungumzia Tamasha hilo Mkuu wa Kitengo cha udhamini na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema kuwa lengo kuu ni kutoa burudani kwa familia na wakazi wa Dar ambao wameendelea kuiunga kampuni hiyo mkono na kuweza kuwaelimisha kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo hivi sasa,kama vile Cheka Nao na Promosheni ya MAHELA inayomwezesha kila mtanzania kushiriki na kujishindia fedha taslimu.
"Tumeandaa burudani hii Mahususi kwa wakazi wa Dar na sehemu zake tukitambua fika kuwa katika msimu huu wa sikukuu familia nyingi hukutana pamoja na kufurahi, hivyo tumeona ni wakati muafaka kutoa burudani kwa wanafamilia,"
Twissa amesema kuwa kufuatia Ofa mpya ya Cheka Nao ambayo inawawezesha wateja wa mtandao huo kupiga simu kwa gharama nafuu kwenda mitandao mingine ambayo imeungwa mkono na Watanzania wengi wameona kuwa ni vyema kuwapa shukurani kwa kuwaburudisha bure.
"Jambo la kipekee ni kuwa sasa wateja wa Vodacom wanaweza kuwasiliana kwa gharama nafuu kwenda mitandao mingine kupitia promosheni yetu ya Cheka Nao, sasa tumeona ni vyema Kucheka pamoja na wateja wetu pale katika fukwe za Coco, alisema Twissa na kuongeza kuwa.
"Kutakuwa na burudani za aina nyingi pamoja na michezo ya watoto hivyo wazazi wawalete watoto wao wakutane na watoto wenzao wacheze pamoja, na pia burudani nyingine kama bembea na michezo ya kuchora,"
Kwa upande wao wasanii watakao toa burudani katika tamasha hilo wamesema kuwa wamejiandaa na kujipanga vyema kuwapagawisha mashabiki watakao jitokeza siku hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa dar es salaam kujitokeza kwa wingi siku hiyo.