CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAM CHADHAMINI FAINALI YA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 
Mratibu wa Masoko wa Chuo cha Uandishi wa Habari School journalism Mass Communication (SJMC) Bi Sophia Ndibalema, akifafanua jambo kuhusiana na Udhamini wa Chuo hicho kwa Washiriki wa Miss Utalii Tanzania, walipotembelea chuo hicho kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali wakati wakijiandaa na Fainali za Taifa 2012/13.

PRESS RELEASE

 
Chuo Kikuu cha Dar es salaam ni miongoni mwa taasisi mbalimbali nchini zilizoitikia wito wa kudhamini fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 ikiwa ni baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa mapungufu mbalimbali ambayo yamepelekea kusogezwa mbele fainali zake kutokana na upungufu na ufinyu wa bajeti kiasi cha shilingi milioni 170 zilizotokana na kushindwa kwa baadhi ya wadhamini kutimiza ahadi zao.
udhamini huo ambao unalenga moja kwa moja kwa washindi, ni pamoja na kulipiwa gharama za ada ya masomo katika musimu wa 2013/14  kozi ya uandishi wa habari  katika chuo kikuu cha dar es salaam ,school of journalism and mass communication( sjmc).
akizungumza jijini dar es salaam kuhusu udhamini huo , rais wa miss utalii tanzania, gideon chipungahelo alisema kwamba ni jambo la kupendeza kwa kuwa kuna ufinyu wa bajeti katika kukamilisha fainali za taifa za miss utalii tanzania.
“tunashukuru kuona taasisi kama chuo kikuu cha dar es salaam kinajitokeza kuunga mkono juhudi za miss utalii tanzania katika harakati za kufanikisha fainali za taifa za miss utalii tanzania 2012/13 ambazo zinalenga kuutangaza utalii wa tanzania, ikiwa ni pamoja na chuo kikuu cha dar es salaam ambacho kina historia ukilinganisha na vyuo vingine katika ukanda wa afrika mashariki na kati, hivyo nazidi kusisitiza kwa wadau, taasisi na makampuni binafsi kujitokeza kuunga na kusaidia juhudi hizi ili fainali za mwaka huu ziwe tofauti na fainali za miaka ya nyuma” alisema chipungahelo
Na kuongza kwamba ahadi kwa wadau na wapenzi wa mashindano haya iko pale pale, kwa kuwa dhamira ipo na nia ya kulifanya shindano la Miss Utalii Tanzania kuendelea kuwa bora na lenye mafanikio makubwa kuliko jingine lolote nchini na afrika iko pale pale, na hili litadhihirika wakati wa fainali kuu ya mashindano mwishoni mwa mwezi huu, hivyo wadau,wafanyabiashara, makampuni binafsi na ya umma, hasa ya kizalendo watakaojitokeza siku hiyo watashuhudia burudani ya aina yake kutoka kwa Warembo mbalimbali wanaowakilisha Mikoa yao,na wawakilishi wa Kanda za Vyuo Vikuu Tanzania bara na Zanzibar.