AMBULANCE AKAMILISHA VIDEO YA 'KAKANYAGA MATOPE'


MSANII anayekuja kwa kasi katika muziki wa bongo Fleva Amos Mwasanje ‘Ambulance’ amekamilisha kurekodi video ya wimbo wake uitwao ‘Kakanyaga Matope’. 
Ambulance amesema kazi ya kurekodi video hiyo iliyofanyika katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam imefanywa na mtayarishaji Fred K . 
Alisema wimbo huo unatarajiwa kuwagusa wengi kutokana na ujumbe ulipo ndani yake, hivyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula. 
Hata hivyo, Ambulance amesema hatoweza kuiachia hewani kwa siku za hivi karibuni kutokana na tatizo la ving’amuzi ambalo kwa sasa ni kilio kwa watanzania wengi ambao wameshindwa kumudu kuvinunua. 
“Nawashukuru mashabiki wa muziki wangu kwa kuendelea kuniunga mkono nawaahidi kuwatayarishia kazi nzuri zaidi, hata hivyo kwa sasa siwezi kuiachia video hiyo mpaka mambo ya ving’amuzi yatakapokaa sawa,’alisema 
Kakanyaga Matope itakuwa ni video ya nne kwa msanii huyo ambapo awali aliachia, Nifundshe Kukatika,Ukienda nyumbani aliomshirikisha Tundaman na Mapepe Kinoma aliomshirikisha Ney wa Mitego.