YANGA YAPUNGUZWA KASI, YAGAWANA POINTI NA MTIBWA SUGAR


TIMU ya Yanga leo imepunguza kasi yake kwenye ligi kuu ya Vodacom baada ya kulazimisa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro katika mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa,Mtibwa ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao lake katika dakika ya 44 kupitia kwa Shaban Kisiga aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Issa Rashid alikipokea pasi ya Osacr Joshua.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo, timu zote ziulifanya mashabulizi ya kupokezana . huku Yanga ikipoteza nafasi za wazi kupitika kwa wachezaji wake Didier Kavumbagu, Jerry Tegete na Simon Msuva, huku Mtibwa nao wakipoteza kupitia kwa Kisiga, Rashid Gumbo, Vicent Barnabas na Hussin Javu.
Hata hivyo, timu hizo zilikwenda mapumziko kwa Mtibwa kuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa kasi zaidi huku Yanga ikionekana na uchu wa kutaka kufunga mabao lakini safu ya ushambuliaji ilishindwa kutikisa nyavu za Mtibwa Sugar.
Hamis Kiiza aliisawazishia Yanga bao katika dakika ya 84, huku Yanga ikiutawala zaidi mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi 33 huku Azam Fc inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 30.
Yanga:Ali Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Athuman Iddy ‘Chuji’, Frank Domayo, Simon Msuva, Didie Kavumbagu, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.
Mtibwa:Hussin Sharif, Said Mkopi, Issa Rashid, Rajab Mohammed, Salum sued, Shabn Nditi, Vicent Barnabas,Rashid Gumbo, Hussein Javu, Shaban Kisiga na Ally M ohammed.

Comments